• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 19-Mei 25)

  (GMT+08:00) 2018-05-25 20:00:01

  UM wapitisha azimio kulaani njaa kama silaha ya vita

  Na hatimaye Um ulionekana kuchukua hatua ya kipekee na inayolenga kuwaokoa raia wa nchi zinazokumbwa na vita pale lilipopitisha azimio kulaani matumizi ya njaa kwa raia kama moja ya njia za vita. Mswada uliopendekezwa na Ivory Coast, Kuwait, Uholanzi na Sweden, unazitaka nchi mbalimbali kufanya uchunguzi kwenye nchi zao kuhusu ukiukaji wa sheria ya kibinadamu ya kimataifa inayohusiana na matumizi ya njaa kwa raia kama moja ya njia za vita.

  Kwa mujibu wa umoja wa mataifa, sehemu kubwa ya watu wanaokabiliwa na tatizo la usalama wa chakula, na asilimia 75 ya watoto waliodumaa wenye chini ya umri wa miaka mitano wanaishi kwenye maeneo yaliyoathiriwa na migogoro, idadi yao ikikaribia milioni 74.

  Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema nchi 10 duniani ndizo zina msukosuko mkubwa wa chakula, ambazo ni Afghanistan, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Iraq, Nigeria, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Syria na Yemen. WFP imelipongeza baraza la usalama kwa kupitisha azimio hilo.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako