• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 19-Mei 25)

  (GMT+08:00) 2018-05-25 20:00:01

  Msichana aliyerhukumiwa kifo Sudan akata rufaa

  Tukielekea nchini Sudan ni kuwa Alhamisi wiki hii Msichana kwa jina Noura Hussein ambaye alihukumiwa kifo kwa kumuua mume wake kutokana na madai ya kumbaka alikata rufaa na kupokelewa na mahakama.

  Mahakama ya Sudan ilimpata na hatia Bi Hussein kwa kuua makusudi mapema mwezi Mei baada ya familia ya mumewe kukataa kufidiwa fedha.

  Hatma ya Bi Hussein ambaye sasa ana miaka 19, ilizua maoni kote duniani na hata kuanzisha kampeni "Haki kwa Noura"

  Baba yake Bi Hussein alimalazimisha kuolewa akiwa na miaka 16 na alikua amejaribu kukimbia.Baada ya ya familia kumkabidhi kwa mume wake, Bi Hussein alisema mume wake aliwaita binamu zake waliomshika huku akimbaka.

  Alimdunga kisu na kumua mumewe wakati alijaribu tena kumbaka siku iliyofuati.Wakati huo huo kundi la wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu la Equality Now limesema kuwa litamwandikia rais Omar al-Bashir kumuomba amuonee huruma.

  Shirika la Amnesty International limesema kuwa hukumu ya mwanamke ya kifo ambaye alikuwa akijitetea inaangazia uzembe wa serikali kukabiliana na ndoa za watoto , ndoa za lazima na ubakaji katika ndoa.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako