• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai30-Julai 6)

    (GMT+08:00) 2018-07-06 19:10:06

    Macron na Buhari wajadili usalama, utamaduni na maendeleo

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwasili Jumanne huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria, ambako alipokelewa na mwenyeji wake wa Nigeria Muhammadu Buhari.

    Katika ziara hiyo rais wa Ufaransa alitembelea klabu ya usiku New Afrika Shrine, iliyofunguliwa mwaka 2000 na mtoto wa mwanamuziki maarufu Fela Kuti.

    Mazungumzo ya muda mrefu kati ya Muhammadu Buhari na Emmanuel Macron yalijikita katika masuala matatu muhimu.

    Mapambano dhidi ya kundi la Boko Haram, kwanza. Katika kuendelea na sera iliyoendeshwa na François Hollande, Emmanuel Macron atasaidia hatua ya jeshi la Nigeria, hasa katika masuala ya upelelezi.

    Kwa upande wa maendeleo ya kiuchumi, Shirika la Maendeleo la Ufaransa litatoa euro milioni 75 kwa ajili ya ugavi wa maji huko Kano, mji mkubwa kaskazini mwa Nigeria. Pia shirika hilo litatoa dola milioni 200 kuboresha usafiri wa mijini Lagos, mji wenye wakaazi milioni 20.

    Kwa upande wa rais wa Ufaransa, Nigeria kwanza ni chaguo la kihisia. Macron aliwahi kuishi nchini Nigeria kwa miaka 15 akifanya kazi katika Ubalozi wa Ufaransa.

    Nigeria pia ni chaguo la kisiasa kutokana na hadhi ya rais Muhammadu Buhari katika eneo la Afrika Magharibi.

    Rais Emmanuel Macron alitembelea klabu ya usiku iliyoanzishwa na aliyekuwa mwanamuziki maarufu Fela Kuti.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako