• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai30-Julai 6)

  (GMT+08:00) 2018-07-06 19:10:06

  Kamanda wa kundi la Al-Shabaab ajisalimisha baada ya uasi wa miaka 8

  Kamanda mwandamizi wa kundi la Al-Shabaab amejisalimisha kwa vikosi vya serikali ya Somalia wiki hii baada ya kuwa muasi kwa miaka 8.

  Jeshi la Taifa la Somalia SNA limesema kamanda wa al-Shabaab Bw. Ali Abdullahi anayeshughulikia eneo la Hajji Muse katika jimbo la Lower Juba, amejisalimisha kwa vikosi vya serikali katika operesheni ya pamoja mjini Bar-Sanguun,

  Kamanda wa divisheni 11 ya jeshi la Somalia Bw. Abdifatah Ibrahim amesema wapiganaji wengine wa kundi hilo pia wamekamatwa katika operesheni hiyo.

  Pia amesema operesheni hiyo imefanywa na kikosi cha AMISOM na jeshi la serikali, baada ya kupata habari za kijasusi zilizosaidia kuwakamata Bw. Abdullahi na mlinzi wake.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako