• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai30-Julai 6)

    (GMT+08:00) 2018-07-06 19:10:06

    Askari wa Gabon kuendelea kubaki Jamhuri ya Afrika ya Kati

    Gabon imeamua askari wake 444 waendelea kubaki nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako wanashiriki katika Ujumbe wa unaosimamia Amani wa Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo inayokabiliwa na mgogoro kwa miaka mitano.

    Taarifa kutoka serikali ya Gabon imesema kwa kuitikia maombi mengi na wito wa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, serikali ya Gabon iatendelea kushiriki katika ulindani wa amani CAR.

    Serikali ya Gabon imesema inafanya hivyo kwa kuonyesha mshikamano wa nchi za kiafrika na uhusiano mzuri wa urafiki na raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Hata hivyo serikali inasema kuwa inashiriki katika kuundaa upya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati katika suala la mafunzo, kwa kuwahudumia maofisa wa jeshi hilo katika shule za jeshi la Gabon.

    Alipokua ziarani mjini Libreville mnamo Juni 14, Rais Touadéra alimwomba mwenzake wa Gabon Ali Bongo Ondimba askari wake kuendelea kushirika katika Minusma.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako