• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai30-Julai 6)

  (GMT+08:00) 2018-07-06 19:10:06

  Watu 800,000 watoroka vurugu Ethiopia

  Machafuko tangu mwezi Juni kusini mwa Ethiopia yamelazimu zaidi ya watu 800,000 kuyatoroka makaazi yao hayo ni kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Ethiopia iliyotolewa Jumatano.

  Mapigano hayo yalitokea mnamo mwe mwaka huu, karibu kilomita 400 kusini mwa mji mkuu, Addis Ababa. Tangu wakati huo, watu zaidi ya milioni 1.2 walilazimika kuyatoroka makaazi yao.

  Mapigano hayo yalichangia kujiuzulu mnamo mwezi Februari wa Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn.

  Waziri mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ambaye aitawazwa mnamo mwezi Aprili, aliahidi kutekeleza mageuzi ya kisiasa na kiuchumi ili kuondokana na mvutano wa kikabila katika jimbo la Oromia ambako yeye hutoka.

  Wakati huo huo Bunge la Ethiopia limepitisha rasimu ya azimio la kuyaondoa makundi matatu ya waasi nchini humo kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.

  Muswada wa rasimu hiyo uliwasilishwa bungeni na baraza la mawaziri la Ethiopia kuyaondoa makundi ya Kundi la ukombozi wa taifa, Kundi la ukombozi wa Oromo na kundi la Ginbot 7.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako