• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai30-Julai 6)

  (GMT+08:00) 2018-07-06 19:10:06

  Rwanda yaadhimisha miaka 24 ya ukombozi

  Rwanda wiki hii iliadhimisha miaka 24 baada ya kupambana na kuikomboa nchi hiyo kwenye utawala mbaya wa zamani na kukomesha mauaji ya kimbari.

  Akihutubia kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Sekta ya Rongi, wilaya ya Muhanga, rais Paul Kagame amesema lengo lao kuu ni kuhakikisha mafanikio ya Warwanda wote.

  Ambapo walishirikiana na wananchi kuikomboa nchi kutoka kwenye utawala mbaya.

  Aidha amewataka wananchi washirikiane na kujenga uchumi ulio imara na endelevu, jumuishi na kuleta mageuzi ya kijamii nchini.

  Shughuli za maadhimisho hayo ya kila mwaka zilianza mwezi Mei ambapo miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha maisha ya watu ilizinduliwa na Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) wakishirikiana na taasisi mbalimbali za umma.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako