• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 4-Agosti 10)

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:18:05

  Emmanuel Ramazani Shadari kuwa kugombea urais kupitia chama tawala DRC

  Joseph kabila wa DR Congo hatowania tena urais na chama chake kimemchagua Emmanuel Ramazani Shadari kuwa mrithi wake na mgombea wa uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba.

  Tayari bwana Ramazani amewasilisha stakhabadhi zake za kuwania urais kwa tume ya ya uchaguzi.

  Emmanuel Shadari mwenye umri wa miaka 57 alikuwa waziri wa maswala ya ndani na ni mwandani wa karibu wa rais Joseph kabila.

  Alikuwa katibu wa kudumu wa chama tawala cha PPRD na mtu muhimu wa kampeni za rais Kabila .

  Wagombea ambao tayari wametangaza kuwa watawania urais ni Jean-Pierre Bemba, 55, mbabe wa zamani wa vita na hasimu wake Kabila ambaye alirejea Kinshasa wiki iliyopita baada ya kuondolewa mashtaka ya uhalifu wa kivita na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya huko Hague.

  Mgombea mwingine wa upinzani Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), naye aliwasilisha makaratasi yake siku ya Jumanne.

  Naye Tryphon Kin-Kiey Mulumba aliyekuwa wakati mmoja msemaji wa Mobutu Sese Seko na ambaye alihudumu mara mbili kama waziri wa serikali ya Kabila ambaya ni mgombea huru.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako