• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 4-Agosti 10)

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:18:05

  Idadi ya waliofariki kwenye tetemeko la ardhi la Indonesia yafikia 82

  Watu zaidi ya 82 wamefariki dunia na mamia wamejeruhiwa katika tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.2 kwenye vipimo vya Richter lililoharibu maelfu ya nyumba na majengo katika kisiwa cha Lombok, katikati ya Indonesia.

  Msemaji wa shirika la taifa la kusimamia majanga Bw. Sutopo Nugroho amesema maelfu ya watu wamekimbia makazi yao, kazi ya kuwaondoa watu walioathirika na tetememo inaendelea na majeruhi wanatibiwa nje ya hospitali ama zahanati kutokana na majengo hayo kuharibiwa au kuwa katika hali hatari.

  Msemaji wa idara ya kudhibiti majanga ya Indonesia amesema nyumba nyingi zimeathirika vibaya, ambapo nyingi kati ya hizo zilijengwa kwa kutumia nyenzo duni.

  Waziri wa mambo ya ndani wa Singapore Kasiviswanathan Shanmugam alikua ziarani katika kisiwa hicho ambapo ametuma picha kwenye mitandao ya kijamii akionyesha namna chumba chake kilivyoathirika.

  Rais wa Indonesia Joko Widodo amesema serikali yake inafanya jitihada za kutosha kunusuru maisha ya majeruhi huku akituma salam za rambirambi kwa familia za wafiwa.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako