• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 4-Agosti 10)

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:18:05

  Jeshi la Israel laimarisha usalama katika eneo la mpaka kati yake na Gaza

  Jeshi la ulinzi la Israel limetoa limeimarisha usalama katika eneo la mpaka kati ya Israel na ukanda wa Gaza ili kuhakikisha usalama wa raia.

  Taarifa hiyo imesema kutokana na taarifa na kitendo cha wapiganaji wa kundi la Hamas, jeshi la Israel limefunga barabara kadhaa zinazoelekea kwenye ukanda wa Gaza katika kusini mwa Israel.

  Pia limeshambulia kituo cha kijeshi cha Hamas, kaskazini mwa eneo la Gaza ikiwa ni kulipiza kisasi kwa kundi hilo kushambulia gari la ufundi la kujenga ukuta wa ulinzi.

  Habari zinasema, jeshi la anga la Israel limeshambulia vituo kadhaa vya kundi la Hamas, baada ya kundi hilo kurusha maroketi zaidi ya 70 na kuwajeruhi watu 6 usiku wa jana.

  Na kwenye tukio linguine Wapiganaji wawili wa kundi la Hamas la Palestina wameuwawa wiki hii katika shambulizi la mizinga lililofanywa na jeshi la Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

  Brigedi ya al-Qassam iliwatambua wapiganaji hao wawili waitwao Ahmed Murjan na Abdul Hafiz al-Selawy kutoka kambi ya wakimbizi ya Jabaliya, kaskazini mwa Gaza.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako