• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 4-Agosti 10)

    (GMT+08:00) 2018-08-10 19:18:05
     

    Saudi Arabia yasitisha biashara na uwekezaji na Canada

    Saudi Arabia imesema kuwa inasitisha biashara na uwekezaji wowote mpya na Canada kwa kuwa inaingilia masuala ya ndani ya taifa hilo la Ghuba.

    Kwenye ujumbe kadhaa kupitia mtandao wa twitter wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Saudi Arabia, ilisema itamfukuza balozi wa Canada na kumuita balozi wake aliye Canada.

    Hatua hii inakuja baada ya Canada kusema kuwa ina wasi wasi kutokana na kukamatwa kwa wapiganiaji kadhaa wa haki za binadamu.

    Kati ya wale waliokamatwa ni mpiganiaji wa haki za wanawake nchini Saudi Arabia Samar Badawi.

    Bi Badawi amekuwa akitoa wito wa kumalizika mfumo wa wanaume kuwasindikiza wanawake kila wanapokwenda.

    Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema haiwezi kamwe kukubali kuingiliwa kwa masuala ya ndani ya nchi yao.

    Ilizungumzia taarifa ya wiki iliyopita ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Canada iliyoitaka Saudi Arabia kuwaachilia mara moja wanaharakati wa kupigania haki za wanawake.

    Serikali ya Canada hadi sasa haijatoa taarifa yoyote kufuatia hatua hizo za kidiplomazia za Saudi Arabia.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako