• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 4-Agosti 10)

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:18:05

  Kiongozi wa juu wa upinzani Zimbabwe akamatwa

  Kiongozi wa juu wa upinzani nchini Zimbabwe Tendai Biti amekamatwa Jumatano wiki hii katika mpaka wa Zambia wakati ambapo chama chake kinaendelea kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.

  Biti amekamatwa kwenye mpaka wa Zambia alipokuwa akijaribu kuvuka mpaka kutafuta hifadhi ya ukimbizi katika nchi hiyo jirani

  Yeye ni mmoja wa viongozi wa juu wa upinzani, na waziri wa zamani wa Fedha wa Serikali ya Umoja wa kitaifa (mnamo mwaka 2009-2013), na sasa anashtumiwa kwa kuchochea vurugu za baada ya uchaguzi.

  Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe (ZEC) ilimtangaza Emmerson Mnangagwa, kuwa alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 50.8.

  Bw Biti alitangaza kabla ya kutangazwa rasmi matokeo ya uchaguzi na Tume ya Uchaguzi kwamba Nelson Chamisa, mgombea wa chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) alishinda uchaguzi, huku akiishtumu Tume ya Uchaguzi kwa kutangaza matokeo tofauti.

  Chama kikuu cha upinzani MDC kimewasilisha kesi Mahakamani kupinga ushindi wa rais Emmerson Mnangangwa.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako