• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 4-Agosti 10)

  (GMT+08:00) 2018-08-10 19:18:05

  Uturuki kuchukua hatua dhidi ya vikwazo kutoka kwa Marekani

  Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki jana huko Ankara amesema Uturuki itafungia mali za waziri wa utekelezaji wa sheria na waziri wa mambo ya ndani wa Marekani zilizoko nchini humo.

  Kitendo hicho kimechukuliwa kuwa ni jibu kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Uturuki.

  Rais Erdogan siku hiyo katika mkutano wa chama cha haki na maendeleo cha Uturuki AKP amesema kuwa, haina sababu kwa Marekani kuweka vikwazo dhidi ya Uturuki ambayo ni mwenzi wake wa kimkakati, na Uturuki haitarudi nyuma kutokana na maneno yenye vitisho na uamuzi wa ujinga.

  Lakini hakutaja majina ya maofisa hao wa Markeani na pia hakuhakikisha kwamba walikuwa na mali nchini Uturuki au la.

  Wakati huo huo Ikulu ya Marekani imetoa taarifa ikitangaza kurudisha tena vikwazo dhidi ya Iran kwenye sekta zisizo za nishati, zikiwemo fedha, chuma, madini, na magari kuanzia tarehe 7.

  Taarifa pia imesema tarehe 5 Novemba Marekani itarudisha tena vikwazo kwenye mambo mengine yanayosalia, ikiwa ni pamoja na mashirika ya kuendesha bandari ya Iran, sekta za nishati, usafirishaji baharini na utengenezaji wa meli, biashara ya mafuta, biashara kati ya mashirika ya fedha ya nchi za nje na benki kuu ya Iran.

  Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema wananchi wa Iran wataifanya Marekani ijute kutokana na kurejesha vikwazo dhidi ya nchi yao.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako