• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 25-Agosti 31)

    (GMT+08:00) 2018-08-31 20:50:29
    Polisi wa Ethiopia wawakamata maofisa 6 waandamizi wa zamani kutoka sehemu ya mashariki yenye machafuko

    Polisi wa Ethiopia wamewakamata maofisa 6 waandamizi wa zamani wa jimbo la Somali lenye machafuko, mashariki mwa nchi hiyo.

    Maofisa hao ni pamoja na Abdijemal Kelonbi aliyekuwa mkuu wa idara ya sheria, Ibrahim Mohammed Mubarak aliyekuwa meya wa Jijiga ambao mji mkuu wa jimbo hilo, na Ibrahim Mehd aliyekuwa ofisa wa idara ya elimu.

    Kabla ya hapo jumatatu wiki hii Bw Abdi Mohammed aliyekuwa kiongozi wa jimbo hilo alikamatwa. Maofisa hao wanashtakiwa kwa tuhuma za ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.

    Tarehe 4 askari wa jeshi la Ethiopia walidhibiti bunge na Televisheni ya jimbo la Somali ili kuuondoa utawala wa Bw. Abdi Mohammed, na kusababisha msukosuko wa kisiasa unaoendelea kwa karibu mwezi mmoja, ambapo wafuasi wa Bw. Mohammed wamefanya vurugu katika miji mbalimbali ya jimbo hilo ukiwemo mji wa Jijiga.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako