Zambia kukabiliwa na ongezeko la wakimbizi kutoka DRC
Zambia inatarajiwa kuwa na ongezeko la idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Kamishna anayeshughulikia mambo ya wakimbizi wa wizara ya mambo ya ndani ya Zambia Bw. Abdon Mawere amesema tayari Zambia imeanza kushuhudia ongezeko la idadi ya wakimbizi.
Akiongea kwenye mkutano mmoja wa wadau wa suala la wakimbizi Bw. Mawere amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, Zambia inatarajiwa kupokea wakimbizi elfu 76, na serikali itaanza kuwahusisha wakimbizi kwenye mipango ya taifa, ili kuwafanya wanufaike na huduma za jamii.
Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR nchini Zambia, Bw. Pierrine Aylara, amesema juhudi za makusudi zinatakiwa kufanyika, ili kuisaidia serikali ya Zambia kukabiliana na tatizo la wakimbizi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |