• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 25-Agosti 31)

    (GMT+08:00) 2018-08-31 20:50:29

    Askari watano wa Kenya wauawa kwa mlipuko

    Askari watano wa Kenya wameuawa kwa mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini lililotengenezwa kienyeji wakati msafara wao ulikua ukielekea katika Kaunti ya Lamu, mashariki mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Somalia, jeshi limesema.

    Tukio hilo lilitokea kilomita chache kutoka mpaka wa Somalia, kati ya vijiji vya pwani ya Kiunga na Sankuri.

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema atahimiza mapambano dhidi ya ugaidi, muda mfupi baada ya wanajeshi watano wa jeshi la Kenya kuuawa na wengine 10 kujeruhiwa kwenye shambulizi la bomu katika mkoa wa pwani.

    Rais Kenyatta ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu wa waliouawa na pole kwa waliojeruhiwa.

    Matumizi ya mabomu yaliyotengenezwa kienyeji dhidi ya polisi na askari wanaopiga doria katika maeneo ya mpakani kaskazini na mashariki mwa Kenya, karibu na Somalia, ynatokea kila kukicha. Wanamgambo wa Kisomali wa Al-Shabab, kwa siku za nyuma wamekuwa wakidai kutekeleza mashambulizi kama haya ambayo yameua maafisa wengi wa usalama na askari wa Kenya.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako