• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 25-Agosti 31)

    (GMT+08:00) 2018-08-31 20:50:29

    Upinzani Sudan Kusini wakubali kusaini makubaliano ya amani

    Kundi kuu la upinzani la Sudan Kusini, SPLM-IO linaloongozwa na Bw. Riek Machar limekubali kusaini makubaliano ya mwisho ya amani baada ya kuyakataa hapo awali.

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw Al-Dirdiri Mohamed Ahmed amesema, baada ya mazungumzo Bw. Machar amekubali kusaini makubaliano hayo tarehe 30 mwezi huu.

    Pia ameahidi kutoa ombi la Bw. Machar kujadili madai yake katika mkutano wa Shirika la Maendeleo ya Kiserikali la nchi za Afrika Mashariki (IGAD).

    Habari zinasema, mazungumzo ya duru ya mwisho ya amani ya Sudan Kusini yalimalizika mapema jana, baada ya serikali na vyama vingine vya nchi hiyo kusaini makubaliano ya kukomesha mgogoro wa ndani.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako