• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 6-Oktoba 12)

  (GMT+08:00) 2018-10-12 16:34:02

  Watu 56 wafariki kwenye ajali mbaya ya barabarani nchini Kenya

  Watu 56 wamefariki wiki hii kwenye ajali mbaya ya barabarani nchini Kenya iliotokea katika eneo la Kericho.

  Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Kaunti ya Kericho, James Mogera, basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 67, lilipoteza mwelekeo barabarani baada ya dereva kushindwa kulimudu, kisha kugonga vizuizi vilivyokuwa kando ya barabara na kubingiria mita 20 kwenye bonde.

  Ajali hiyo ilitokea jumatano saa 11 alfajiri, na kati ya wahanga wa ajali hiyo, 15 ni wanawake na wengine 32 ni wanaume, watu 15 wamenusurika.

  Mmoja wa abiria walionusurika amesema dereva hakuheshimu sheria za usalama barabarani.

  Polisi wamemkamata dereva wa basi hilo mwenye umri wa miaka 72 ambalo halikuwa na bima husika.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako