• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 6-Oktoba 12)

  (GMT+08:00) 2018-10-12 16:34:02

  Rais wa Marekani asema mkutano wa pili kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini utafanyika baada ya uchaguzi mdogo

  Rais Donald Trump wa Marekani akiwa jimboni Iowa amesema, kutokana na kushughulikia uchaguzi, mkutano wa pili kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un utafanyika baada ya uchaguzi mdogo wa nchi hiyo utakofanyika Novemba 6.

  Kabla ya hapo, rais Trump alisema kuwa ziara ya waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Mike Pompeo nchini Korea Kaskazini na mazungumzo kati yake na Bw. Kim vilipata mafanikio. Amesema nchi hizo mbili zinaandaa mkutano wa pili wa viongozi, na tayari sehemu kama nne zimependekezwa kwa ajili ya mkutano huo, lakini ana hakika kuwa mkutano huo hautafanyika nchini Singapore.

  Bw. Pompeo pia amesema, ziara yake imepata maendeleo halisi, na ingawa pande mbili zina kazi nyingi za kufanya, lakini zimeweza kuona njia ya kutumiza Korea Kaskazini kuondoa silaha za kinyuklia kwa pande zote.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako