• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 6-Oktoba 12)

    (GMT+08:00) 2018-10-12 16:34:02

    Agnes Reeves Taylor, akana mashitaka yanayomkabili

    Aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor-Agnes Reeves Taylor, amekana mashtaka ya mateso wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia katika miaka ya 1990, wakati alipokuwa akisikilizwa mbele ya mahakama ya jinai ya London, nchini Uingereza.

    Agnes Reeves Taylor, mwenye umri wa miaka 52, anatuhumiwa kuhusika katika vitendo vya mateso dhidi ya watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na watoto, " alipokuwa akishikiliwa nyadhifa mbalimbali."

    Pia anatuhumiwa kuwa alishinikiza majeshi ya Charles Taylor, National Patriotic Front of Liberia (NPFL), kutumia ubakaji wa wanawake kama njia ya mateso.

    Agnes Reeves Taylor, aliyekuwa mhadhiri katika Chuko Kikuu cha English Coventry University, anaishi katika mji wa Dagenham, mashariki mwa London, na kwa sasa yuko chini ya ulinzi katika gereza la Bronzefield, kusini-mashariki mwa Uingereza.

    Charles Taylor na Agnes Reeves Taylor walitalakiana mnamno mwaka 1996. Kisha kiongozi huyo wa waasi alichukua hatamu ya uongozi kama rais wa Liberia kuanzia mwaka 1997 hadi 2003.

    Alihukumiwa na Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCSL) katika miaka ya 2012 kifungo cha miaka 50 kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa katika nchi jirani ya Liberia ya Sierra Leone.

    Charles Taylor anatumikia kifungo cha miaka hamsini katika jela la Uingereza.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako