• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 6-Oktoba 12)

  (GMT+08:00) 2018-10-12 16:34:02

  Mwanasiasa wa Rwanda aliyeachiwa ahojiwa kutokana na kusema hukumu dhidi yake ni ya kisiasa

  Idara ya upelelezi ya Rwanda RIB imemhoji mwanasiasa mwanamke aliyeachiwa huru mwezi Septemba kwa msamaha wa rais, kutokana na kauli zake kuwa hukumu dhidi yake ilikuwa ni ya kisiasa.

  Taarifa iliyotolewa na RIB inasema Bibi Victoire Ingabire alifika katika ofisi ya RIB mjini Kigali baada ya kuitwa kujadili taarifa zisizo sahihi alizotoa hivi karibuni, ambazo zinaweza kuchukuliwa kuwa makosa kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai.

  Taarifa inasema Bibi Ingabire alihojiwa kutokana na kauli kuwa hukumu dhidi yake ilikuwa ni "ya kisiasa" na kuwataja wafungwa wengine kuwa ni "wafungwa wa kisiasa".

  Bibi Victoire Ingabire ambaye ni kiongozi wa chama cha kisiasa kisichosajiliwa cha FDU-Inkingi, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 mwaka 2013 na mahakama kuu ya Rwanda, baada ya kukutwa na hatia ya kupanga njama kuihujumu nchi kupitia ugaidi, na kutweza ubaya wa mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 dhidi ya watutsi nchini Rwanda.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako