Walimu wawili wauawa katika wilaya ya mpakani nchini Kenya
Waalimu wawili wa shule ya sekondari ya wavulana Arabia iliyoko Mandera Mashariki, kaskazini mashariki mwa Kenya wameuawa na watu wenye silaha ambao walivamia shule hiyo Jumtano alfajiri.
Kamishna wa kanda ya kaskazini mashariki ya Kenya Bw. Mohamed Birik amesema, polisi wanawasaka washambuliaji hao ambao pia walichoma moto chumba cha walimu cha shule hiyo.
Walimu wengi wamekimbia eneo hilo kwa hofu ya shambulizi zaidi kutoka kwa wapiganaji ambao wanawalenga walimu wasio wenyeji wanaofanya kazi kwenye eneo hilo.
Shambulizi hilo limetokea umbali mfupi kutoka sehemu ambayo washambuliaji waliwaua waalimu 28 Novemba mwaka 2014.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |