Cyril Ramaphosa ateua Tito Mboweni kuwa Waziri mpya wa fedha
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemteua Tito Mboweni kuwa Waziri mpya wa fedha.
Gavana huyo wa zamani wa Benki Kuu, anachukua nafasi ya Nhlanhla Nene aliyejiuzulu siku ya Jumanne baada ya madai kuwa alishirikiana kwa karibu na familia ya kitajiri ya Gupta katika masuala ya kibiashara.
Rais Ramaphosa alikubali kujiuzulu kwake baada ya wiki iliyopita, akiwa mbele ya tume maalum inayochunguza visa vya ufisadi, kukiri uhusiano wake wa kibiashara na familia hiyo.
Familia ya Gupta imekuwa ikihusishwa na rais wa zamani Jacob Zuma, ambaye serikali yake ilituhumiwa kutekwa na familia hiyo.
Waziri huyo wa zamani alisema alikataa kupokea fedha wakati wa uongozi wa rais wa zamani Zuma, wakati serikali yake ilipokuwa inakabiliwa na madai ya ufisadi.
Zuma ambaye amefikishwa Mahakamani kwa madai mbalimbali ya ufisadi, ameendelea kukataa kuhusika na wizi wa fedha za umma akishirikiana na familia hiyo ya tajiri lakini pia alipokuwa Waziri miaka ya tisini.
Ramaphosa amesema serikali yake haitakubali visa vya ufisadi kuendelea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |