• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 1-March 8)

    (GMT+08:00) 2019-03-08 17:53:33

    Rais wa Iran apongeza vikosi vya usalama vya Iraq kwa kushinda ugaidi

    Rais Hassan Rouhani wa Iran amepongeza kurejea kwa usalama na utulivu nchini Iraq baada ya nchi hiyo kuwashinda wapiganaji wa kundi la IS.

    Rais Rouhani amesema hayo alipokutana na Spika wa Bunge la Iraq Mohamed al-Halbousi ambaye yuko ziarani nchini Iran. Amesema nchi yake iko tayari kuongeza uhusiano na Iraq katika nyanja mbalimbali na kutoa wito wa kuimarisha zaidi uhusiano wa karibu na wa kindugu na Iraq.

    Kwa upande wake, al-Halbousi ameshukuru msaada wa Iran kwa Iraq katika kupambana na ugaidi. Amesisitiza kuwa, maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili yanasaidia utulivu katika eneo hilo, na kurejea tena nchi yake kupinga vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako