• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 1-March 8)

    (GMT+08:00) 2019-03-08 17:53:33

    Rais wa Ufaransa kuzuru Djibouti, Ethiopia na Kenya

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajia kuanza ziara ndefu barani Afrika ambapo ataanzia nchini Djibouti Machi 11 kabla ya kuelekea nchini Ethiopia Machi 12 na baadaye nchini Kenya.

    Masuala ya kimkakati, kiuchumi, kiutamaduni na hali ya hewa ndivyo vilivyowekwa kwenye orodha ya ziara hii ya kwanza ya rais huyo katika Pembe ya Afrika.

    Hatua ya kwanza ya ziara hii ilitangazwa kwa kuchelewa. Emmanuel Macron ataanza safari yake ya Machi 11 nchini Djibouti ambako atakuwa na kikao na rais wa nchi hiyo Ismaïl Omar Guelleh kabla ya kuzuru kambi ya wanajeshi wa Ufaransa ambayo inajumuisha idadi kubwa ya wanajeshi wa Ufaransa nje ya taifa hilo

    Hii ni ziara ya kimkakati nchini Djibouti kutokana na kwamba nchi hiyo inapokea vituo vya kijehi kutoka katika mataifa makubwa yenye nguvu duniani kama vile (Marekani, Japan, Ujerumani, Italia na hivi karibuni China) - na ni mshirika mkubwa wa kihistoria.

    Emmanuel Macron atakuwa ni rais wa pili wa Ufaransa, baada ya Nicolas Sarkozy mwaka 2010, kwenda nchini Djibouti baada ya miaka ishirini.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako