Kenya yasema huduma za ndege zarejea kama kawaida kwenye uwanja wa ndege wa Nairobi
Mamlaka ya viwanja vya ndege ya Kenya (KAA) imesema, huduma za ndege zilizoathiriwa na mgomo uliofanywa kinyume cha sheria na baadhi ya wafanyakazi wa uwanja wa ndege, zimerudi katika hali ya kawaida.
KAA imesema ndege zote zilizotarajiwa kufika kwa mujibu wa ratiba zilishughulikiwa, na ndege zilizochelewa kuondoka kutokana na mgomo ziliondoka.
Taarifa iliyotolewa na KAA inasema mamlaka hiyo inaendelea polepole kurudisha shughuli za kawaida kwenye uwanja wa Jomo Kenyatta JKIA, wakati huo huo imewashauri abiria wawasiliane na mashirika ya ndege ili kuthibitisha mipango yao ya safari.
Awali wiki hii Shughuli za safari za ndege zilikwama katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, baada ya wafanyikazi wanaotoa huduma mbalimbali katika uwanja huo kugoma.
Mgomo huo ulianza saa tisa usiku wa jumatano, kwa kile wafanyikazi hao wanalalamikia uongozi wa usimamizi wa shughuli za usafiri katika uwanja huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |