• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 1-March 8)

    (GMT+08:00) 2019-03-08 17:53:33

    Kabila na Tshisekedi wakubaliana kuunda serikali ya muungano

    Washiriki wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi pamoja na wale wa mtangulizi wake, Joseph Kabila, Jumatano wiki hii, wamekubaliana kuhusu uundwaji wa serikali ya muungano wa kitaifa.

    Hatua hii inafungua njia kuelekea uteuzi wa mtu ambaye atakabidhiwa jukumu la kufanikisha upatikanaji wa Waziri Mkuu, Vyombo vya habari nchini DRC vimeripoti.

    Katika hatua nyingine kiongozi wa Upinzani wa Lamuka Martin Fayulu, na Mkurugenzi mkuu wa ofisi ya rais Vital Kamerhe wamekataa kushiriki vikao vya Bunge.

    Martin Fayulu anasema suala hilo haliingii akilini yeye kama rais aliyechaguliwa na wananchi haina maana yeye kuitwa mbunge, nchini humo.

    Hata hivyo Kanisa Katoliki nchini DRC limeendelea kusema kuwa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi DRC (CENI) hayaendani na ukweli halisi wa matokeo ya uchaguzi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako