• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 1-March 8)

    (GMT+08:00) 2019-03-08 17:53:33

    Aliyekuwa meneja wa kampeni za Trump afungwa

    Meneja wa zamani wa kampeni za rais wa Marekani Donald Trump Paul Manafort amehukumiwa kifungo cha miezi 47 jela kwa udanganyifu katika ulipaji wa kodi na benki.

    Alipatikana na hatia mwaka jana kwa kuficha mamilioni ya dola wakati alipokuwa balozi nchini Ukraine.

    Anatarajiwa kuhukumiwa katika kesi nyingine wiki ijayo kwa kufanya kampeni kinyume cha sheria.

    Mashitaka hayo yalitokana na na uchunguzi uliofanyika juu ya ikiwa maafisa wa kampeni ya Trump walifanya njama na Urusi ili kumuwezesha apate ushindi katika uchaguzi wa 2016.

    Balozi maalumu wa wizara ya sheria ya Marekani Robert Mueller anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake wa miezi 22 ambao unalenga urais wa Trump.

    Manafort atalazimika pia kulipa marejesho ya dola milioni $24 pamoja na faini ya dola $50,000.

    Manafort mwenye umri wa miaka 69-aliiambia mahakama Alhamisi jioni katika mji wa Alexandria, Virginia, kwamba " miaka miwili iliyopita imekuwa migumu sana katika maisha yake .


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako