• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 1-March 8)

    (GMT+08:00) 2019-03-08 17:53:33

    Ethiopia na washirika wake watoa mwito wa msaada wa dola bilioni 1.3 kwa watu milioni 8.3 kwa mwaka huu

    Serikali ya Ethiopia na washirika wa kibinadamu wametoa mwito wa msaada wa dola za kimarekani bilioni 1.3 ili kukidhi mahitaji ya dharura ya watu milioni 8.3.

    Mwito huo ulitolewa mjini Addis Ababa wakati serikali ya Ethiopia na washirika wa kibinadamu walipozindua mpango wa pamoja wa kukabiliana na hali ya kibinadamu nchini Ethiopia.

    Kwa mujibu wa mpango huo, watu milioni 4.4 wanahitaji msaada wa lishe, ikiwa ni pamoja na watoto zaidi ya laki 6 wenye umri wa chini ya miaka mitano, ambao wanahitaji matibabu ya utapiamlo mkali (SAM).

    Watu milioni 2.7 waliopoteza makazi na waliorudi nyumbani watanufaika na makazi ya dharura na msaada usio chakula, na mamilioni ya watu watapata msaada wa afya ya dharura, maji, elimu, ulinzi na kilimo hadi mwishoni mwa mwaka.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako