• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 9-March 15)

  (GMT+08:00) 2019-03-15 18:54:14
  Watu 49 wauwawa kwenye mashambulizi dhidi ya misikiti New Zealand

  Watu 49 wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa vibaya ijumaa baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch, huko New Zealand.

  Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amelitaja shambulio hilo kuwa limeleta 'kiza kikubwa' nchini humo.

  Kamishna wa polisi Mike Bush anasema Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa, , lakini ameonya kwamba huenda washukiwa zaidi wapo.

  Inaarifiwa kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali.

  Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.

  Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa "gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia".

  Walioshuhudia mkasa huo wameambia vyombo vya habari kwamba walilazimika kutoroka kuokoa maisha yao na waliona watu walioanguka chini wanaovuja damu nje ya mskiti wa Al Noor.

  Maafisa wameshauri misikiti yote katika mji huo ifungwe mpaka ilani itakapotolea, wakieleza kwamba hili lilikuwa shambulio la vurugu ambalo halikutarajiwa.

  Bado haijulikani wazi nini kilichofanyika ndani ya misikti hiyo, taarifa mpaka sasa zimetoka kwa walioshuhudia mkasa na waliozungumza na vyombo vya habari.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako