• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 9-March 15)

  (GMT+08:00) 2019-03-15 18:54:14

  Wapiganaji 16 wa kundi la Al-Shabaab wauawa kusini mwa Somalia

  Wapiganaji 16 wa kundi la Al-Shabaab la Somalia wameuawa katika mapigano kati ya kundi hilo na jeshi la Somalia yaliyotokea kwenye eneo kati ya Bar Sanguni na Jamame mkoani Lower Juba, kusini mwa Somalia.

  Msemaji wa usalama mkoa wa Jubaland Bw. Abdi Nur Ibrahim amesema, shambulizi hilo lilifanywa na jeshi la Somalia kwa pamoja na vikosi vya usalama vya mkoa huo na wenzi wa kimataifa.

  Wakati huohuo, jeshi la ulinzi la Kenya (KDF) chini ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika kimewaua wapiganaji watatu wa kundi la Al-Shabaab na kumkamata mwingine mmoja katika shambulizi la kurushiana risasi lililotokea kwenye mkoa wa mpakani wa Bura Hache.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako