• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 9-March 15)

  (GMT+08:00) 2019-03-15 18:54:14

  Mkutano wa nne wa Mazingira wa UM wapitisha mipango ya kukabiliana na changamoto zinazokabili mazingira

  Mkutano wa nne wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa umekamilika ijumaa mjini Nairobi, Kenya.

  Mkutano huo wa siku tano umehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 4,700 kutoka nchi na sehemu 170 duniani na wamejadili njia mbalimbali za kutatua masuala ya mazingira, na kutimiza matumizi na uzalishaji endelevu.

  Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni waziri wa mazingira wa Estonia Bw. Siim Kiisler, amesema miaka minne iliyopita, dunia imeshuhudia maafa mbalimbali yakiwemo mafuriko makubwa na ukame, ambavyo vimesababisha vifo vingi vya watu.

  Maamuzi yalioyopitishwa kwenye mkutano huo yataathiri kwa kina utekelezaji wa Makubaliano ya Paris na Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030, na kuondoa vikwazo kwa Mkutano wa kilele wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa ya Umoja wa Mataifa wa mwaka huu.

  Kaimu mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Bibi Joyce Msuya amesema kwenye mkutano huo kuwa dunia inapaswa kuchukua hatua haraka ili kupunguza utoaji wa hewa za Kaboni Dioxide, na kuendeleza uchumi usio na uchafuzi wa mazingira.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako