• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 9-March 15)

    (GMT+08:00) 2019-03-15 18:54:14

    Rwanda yapiga marufuku Boeing 737 Max katika anga yake

    Shirika la usafiri wa ndege Rwanda limetoa agizo kwa marubani na kampuni za ndege kutoendesha ndege za Boeing 737 Max 8 ana 9 katika anga ya Rwanda.

    Rwanda sasa imejiunga na mataifa mengine duniani ambayo yamepiga marufuku usafiri wa ndege hizo za aina ya Boeing 787 Max 8 na Max 9.

    Hii inafuata ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines Jumapili ilioanguaka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa na kusababisha vifo vya watu 157.

    Taarifa zinaeleza kwamba Rwanda ilikuwa na mipango ya kukodisha ndege mbili za aina hiyo Boeing 737- 800.

    Hatahivyo, huenda mipango hiyo ikasitishwa kwa muda sasa wakati kukisubiriwa uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka Jumapili nje kidogo ya mji mkuu Addis Ababa.

    Ndege kama hiyo ya kampuni ya Lion Air, ilianguka kutoka pwani ya Indonesia Oktoba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 189.

    Katika taarifa rasmi iliyowekwa kwenye mtandao wa twitter ya mkurugenzi mkuu katika shirika hilo la usafiri wa ndege Rwanda, Silas Udahemuka, RCAA limesema kwamba marufuku hiyo imeanza kufanya kazi mara moja.

    Marekani pia imekuwa nchi ya hivi karibuni kusitisha usafiri wa ndege hiyo ya Boeing 737 Max yakiwemo mataifa mengine kama Uingereza, Umoja wa Ulaya, China India na Australia ambayo yote yameamua kusitisha usafiri wa ndege hizo.

    Ndege zote za Boeing 737 Max 8 na 9 zimepigwa marufuku kuhudumu hadi angalau Mei baada ya ajali hiyo ya shirika la ndege la Ethiopia, Shirika la kitaifa la usafiri wa ndege nchini Marekani (FAA) limesema.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako