• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 4-Mei 10)

  (GMT+08:00) 2019-05-10 20:15:06
  Watu 50 wafariki baada ya lori la mafuta kulipuka Niamey

  Mlipuko wa lori ya mafuta umeua watu hamsini na tano na kuwajeruhi wengine zaidi ya thelathini, mita chache kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Niamey.

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Niger amesema ajali hiyo ilitokea usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii karibu na mji mkuu wa Niger, Niamey.

  Idadi ya watu waliofariki dunia ni55 na 36 walijeruhiwa.

  Lori lililokuwa limesheheni mafuta lilianguka kwenye barabara ya reli, nje ya mji wa Niamey.

  Watu walikuwa wakijaribu kuchota petroli iliyokuwa ikimwagika kutoka kwenye tenki ya lori hilo wakati mlipuko ulipotokea.

  Nyumba zilizo karibu na eneo la tukio ziliharibika vibaya.

  Hata hivyo shughuli kwenye uwanja wa ndege zimeendelea kama kawaida.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako