• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 4-Mei 10)

  (GMT+08:00) 2019-05-10 20:15:06

  Kikundi cha mawasiliano ya kimataifa cha suala la Venezuela chahimiza kutatua mgogoro wa nchi hiyo kwa njia ya amani

  Mkutano wa tatu wa Kikundi cha mawasiliano ya kimataifa cha suala la Venezuela umefanyika huko San Jose, Costa Rica, na kutoa wito wa kutatua mgogoro wa Venezuela kwa njia ya amani.

  Mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bibi Federica Mogherini amezihimiza pande mbalimbali kuepusha hali ya wasiwasi kupamba moto, na kupinga kuingilia mambo ya Venezuela kwa njia ya kijeshi, huku akisisitiza kuwa utatuzi pekee ni kutafuta njia ya kisiasa ya kidemokrasia na amani na kuheshimu nia ya watu wote wa nchi hiyo.

  Habari nyingine zinasema, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inapenda kuimarisha mawasiliano na jumuiya ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Ulaya, na kutoa mchango wa kiujenzi kwa pamoja ili kupata utatuzi wa kisiasa wa suala la Venezuela.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako