• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 4-Mei 10)

  (GMT+08:00) 2019-05-10 20:15:06

  Somalia kuandikisha polisi 400 ili kulinda usalama wa barabara kuu

  Polisi 400 wataandikishwa katika jimbo la kusini magharibi nchini Somalia ili kusaidia kuimarisha usalama kwenye njia za usambazaji na kuwezesha usafirishaji huru wa misaada ya kibinadamu.

  Maofisa wamesema tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imetoa mafunzo kwa maofisa wa jimbo la kusini magharibi ambao watawafanyia ukaguzi watu wanaotaka kujiunga na jeshi la polisi, watu ambao pia watasaida kutoa ulinzi kwenye maeneo ya makazi ya watu.

  Mratibu wa mageuzi ya polisi wa AMISOM Bw. Maxwell Chikunguru amesema mchakato wa kuwakagua watu hao, utasaidia kuandikisha watu wanaofaa.

  Mwaka 2017 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha uamuzi wa kupunguza polepole majukumu ya AMISOM nchini Somalia, na hatimaye kuondoka kabisa mwaka 2021. Bw. Chikunguru amesema jukumu lao kwa sasa ni kulijengea uwezo jeshi la polisi la Somalia.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako