• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 4-Mei 10)

    (GMT+08:00) 2019-05-10 20:15:06

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani afanya ziara ya ghafla mjini Baghdad

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo wiki hii alifanya ziara ya ghafla mjini Baghdad, na kuitaka serikali ya Iraq ikabiliane na "tishio" la Iran, ili kuhakikisha maslahi ya Marekani nchini Iraq.

    Ziara yake ya saa nne iliamuliwa ghafla na Bw. Pompeo baada ya kufuta safari yake nchini Ujerumani. Akizungumzia sababu ya safari hiyo, amesema kikosi cha Iran kinazidisha shughuli zake, ambazo ni dalili ya tishio la kufanya shambulizi.

    Bw. Pompeo amezungumza na wanahabari baada ya kukutana na rais Barham Salih wa Iraq na waziri mkuu Bw. Adil Abdul-Mahdi, akisema wamezungumza kuhusu umuhimu wa kuhakikisha maslahi ya Marekani nchini Iraq, na viongozi wa Iraq wameahidi kuwa ni wajibu wao kuhakikisha maslahi ya Marekani. Ameongeza kuwa Marekani inaihimiza serikali ya Iraq idhibiti nguvu zote husika zenye uhusiano wa karibu wa kidini na Iran.

    Awali wiki hii Ikulu ya Marekani ilitangaza kuwa nchi hiyo inaweka vikwazo dhidi ya sekta za chuma, chuma cha pua, alumini na shaba nchini Iran. Taarifa iliyotolewa na rais Donald Trump inasema sekta hizo zinailetea Iran fedha nyingi za kigeni zikifuata mafuta ghafi, na Marekani itaiwekea Iran vikwazo zaidi kama nchi hiyo haitabadili mwenendo wake. Vikwazo hivyo ni pamoja na hatua mpya ya Marekani ya kutoa shinikizo kubwa zaidi dhidi ya Iran, ambayo inakuja mwaka mmoja baada ya serikali ya sasa ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran mwezi Mei mwaka jana.Lakini wakati huo huo msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, kulinda na kutekeleza kwa pande zote makubaliano ya nyuklia ya Iran ni majukumu ya pamoja ya pande mbalimbali, China inazihimiza pande husika kujizuia na kuimarisha mazungumzo, ili kuepusha kupamba moto kwa hali ya wasiwasi.

    Serikali ya Iran imesema kutokana na Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya suala la nyuklia la Iran, itatangaza kusimamisha baadhi ya ahadi za makubaliano hayo, lakini haitajitoa kabisa.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako