• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 31-Septemba 6)

  (GMT+08:00) 2019-09-06 18:50:48

  Robert Mugabe afariki

  Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia.

  Mmoja wa wanafamilia amethibitishia kuwa, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95. Mugabe alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu.

  Ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong'olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi. Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa tayari amethibitisha kupitia mtandao wa twitter juu ya taarifa za kifo hicho.

  Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 kwenye koloni la Rhodesia.

  Alitupwa jela kwa miaka 10 bila ya kufunguliwa mashtaka kwa kuukosoa uongozi wa Rhodesia mwaka 1964.

  Mwaka 1973, yungali gerezani alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Zimbabwe African Union (Zanu), ambacho alikuwa ni mwanachama mwanzilishi.

  Baada ya kuachiwa kutoka gerezani, alikimbilia Msumbiji na kuongoza mapambano ya kijeshi ya kudai uhuru.

  Licha ya kuwa mpiganaji wa vita vya kushtukiza, alisifika kwa kuwa mzuri kwenye majadiliano.

  Mwaka 1980 akafanikiwa kuingia madarakani baada ya uchaguzi uliomaliza utawala wa walowezi wachache wa kizungu.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako