• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 31-Septemba 6)

    (GMT+08:00) 2019-09-06 18:50:48

    China yasema wazo la wanasiasa husika wa Marekani la kuivuruga Hong Kong laonekana wazi

    Ofisi ya Kamisheni ya wizara ya mambo ya nje ya China mkoani Hong Kong imesema, China inapinga vikali hoja na vitendo vya wanasiasa husika wa Marekani wanaopuuza hali halisi, kuchanganya mema na mabaya na kuingilia kati mambo ya Hong Kong na siasa ya ndani ya China.

    Habari zinasema, mwenyekiti wa kamati ya mambo ya kidiplomasia ya baraza la chini la bunge la Marekani Bw. Elliott Engel na mbunge Bw. Michael McCaul wametoa taarifa ikidai watu wenye msimamo mkali wanaofanya vitendo vya kimabavu wameonesha ujasiri unaoheshimiwa, huku wakichafua sera ya China kwa Hong Kong na kuingilia utekelezaji wa sera wa serikali ya mkoa wa Hong Kong.

    Msemaji wa kamisheni hiyo amesema, vitendo vya baadhi ya watu wenye msimamo mkali ni viovu na vya kikatili sana, hivyo polisi wa Hong Kong wamelazimika kutumia nguvu ya kiwango cha chini ili kulinda utulivu wa jamii.

    Amesema mtu yeyote asiye na upendeleo anaweza kutambua upande upi umefanya makosa, na kwamba wabunge husika wa Marekani wamesema uwongo kwa kupuuza hali halisi na kupamba vitendo vya kimabavu huku wakikosoa utekelezaji halali wa sheria wa polisi wa Hong Kong. Aidha amesisitiza kuwa vigezo viwili vya unafiki na mantiki ya wizi vinalaaniwa na kila mtu mpenda haki.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako