• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 31-Septemba 6)

  (GMT+08:00) 2019-09-06 18:50:48

  Nigeria yasusia mkutano wa kiuchumi Afrika Kusini huku wito ukitolewa kukomeshwa mashambulizi dhidi ya wageni

  Nigeria imesema haitatuma mwakilishi katika mkutano wa kiuchumi wa dunia unaoendelea nchini Afrika Afrika, kufuatia mashambulizi na uvamizi unaendelea kulenga maduka ya wageni nchini humo.

  Makamu wa rais Yemi Osinbajo alitarajiwa kuhotubia mkutano huo mjini Cape Town Alhamisi lakini hakuwepo.

  Watu zaidi ya sita wameauwa kutokana na vurugu hizi zilizoanza kushuhudiwa wiki hii, jijini Johannerburg na baadaye kwenda jijini Pretoria.

  Nchini Nigeria, Jumatano wiki hii kulikuwa na maandamano, raia wa jiji kuu Abuja wakiandamana na kuvamia maduka ya wawekezaji kutoka Afrika Kusini kama MTN na duka la jumla la Shoprite, kwa kile walichosema ni kulipiza kisasi

  Umoja wa Afrika umelaani chuki dhidi ya wageni na kusababisha ghasia nchini Afrika Kusini. Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki, amelaani ghasia hizo lakini akaongeza kuwa ametiwa moyo na hatua zilizochukuliwa na Afrika Kusini za kuwakamata watuhumiwa.

  Wakati huo huo shirikisho la mpira wa miguu la Zambia FAZ, limefuta mechi ya kirafiki iliyokuwa ifanyike mjini Lusaka siku ya Jumamosi kutokana na vurugu hizo. Kwenye taarifa yake iliyoitoa Jumanne, FAZ imesema sababu za kusitisha mechi hiyo ni hali ya kiusalama nchini Afrika Kusini, hata kama Zambia ilikuwa mwenyeji.

  Waziri anayeshughulikia maswala ya Polisi Bheki Cele anasema wanapambana na watu wanaoshambulia maduka ya wageni.

  Rais Cyril Ramaphosa amelaani mashambulizi dhidi ya wageni na uvamizi wa maeneo yao ya biashara jijini Johhanersburg.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako