• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 31-Septemba 6)

    (GMT+08:00) 2019-09-06 18:50:48

    WHO yapeleka dozi 300 za chanjo ya Ebola magharibi mwa Uganda

    Shirika la Afya Duniani WHO limepeleka dozi 300 za chanjo ya Ebola kwa ajili ya kuwapatia chanjo watu wote waliowasiliana na mshichana mwenye umri wa miaka 9 aliyefariki kwa Ebola wilayani Kasese, nchini Uganda, kufuatia mlipuko wa pili wa ugonjwa huo.

    Mwakilishi wa WHO nchini Uganda Yonas Tegegn Woldemariam, amewaambia wanahabari kuwa chanjo hiyo itatumika kwa wale wote waliowasiliana na kumhudumia mtoto huyo katika kitengo cha matibabu ya Ebola cha hospitali ya Bwire. Kwa mujibu wa waziri wa afya wa Uganda Joyce Moriku Kaducu, watu wanne waliosafirishwa kwenye gari moja ya wagonjwa na mtoto huyo walirejeshwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki hii ili kupewa chanjo na kufuatiliwa zaidi.

    Wakati huohuo Shirika la Kuwahudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema tangu ugonjwa wa Ebola ulipuke kaskazini mashariki mwa DRC mwaka mmoja uliopita, karibu watoto 600 kati ya 850 waliokumbwa na ugonjwa huo wamefariki. Hata hivyo shirika hilo limesema kwa mara ya kwanza sasa wamekuwa na njia ya kuzuia na kutibu ugonjwa huo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako