• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 31-Septemba 6)

  (GMT+08:00) 2019-09-06 18:50:48

  Rais wa Iran atangaza Iran itaendelea kusimamisha utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia

  Shirika la habari la Iran limemkariri kiongozi mkuu wa nchi hiyo Ali Khamenei akisema kuwa, Iran itaendelea kusimamisha utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia. Pia amesema Iran itatangaza mapema hatua za kusimamisha utekelezaji wa makubailano hayo katika kipindi cha tatu. Akisisitiza kuwa hatua hizo mpya zitaleta athari muhimu.

  Ofisa wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran aliwahi kusema kuwa, endapo nchi nyingine zinazohusika hazitekelezi wajibu ipasavyo, Iran ina uwezo wa kurejesha urutubishaji wa uranium ndani ya siku mbili.

  Huku hayo yakijiri wiki hii Marekani imetangaza kuwa imeweka vikwazo dhidi ya mashirika ya anga ya Iran kufuatia hali ya wasiwasi.

  Vikwazo hivi vipya vinalenga Idara ya anga ya Iran na taasisi zake mbili za utafiti, ambavyo ni vya mwanzo kati ya vile vitakavyotangazwa na Marekani wakati hali ya wasiwasi inazidi kuongezeka katika Mashariki ya Kati. Rais Hassan Rouhani wa Iran tayari ameondoa uwezekano wa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani juu ya mpango wa nyuklia wa Iran.

  Akihutubia kwenye kikao cha wazi cha bunge la Iran, rais Rouhani, amesema hawajawahi kutoa uamuzi wa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani wakati wowote ule. Lakini, amesisitiza kuwa kama Marekani ikiondoa vikwazo dhidi ya Iran, itawezekana kwa nchi hiyo kuhudhuria mazungumzo ya nchi tano pamoja na Ujerumani.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako