• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 31-Septemba 6)

  (GMT+08:00) 2019-09-06 18:50:48

  Umoja wa Mataifa waonya kuwa hali ya usalama wa chakula inazidi kuwa mbaya nchini Sudan na Somalia

  Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uratibu wa mambo ya kibinadamu OCHA imeeleza wasiwasi kuhusu kukosekana kwa usalama wa chakula nchini Sudan na Somalia.

  Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, watu wapatao milioni 6.3 ambao ni asilimia 14 ya watu wote wa Sudan wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, ukiwa ni msukosuko mbaya zaidi tangu kuanzishwa kwa Mpango wa usalama wa chakula nchini humo mwaka 2007.

  Nchini Somalia, mvua zinazochelewa na zisizokuwa na uhakika mwaka huu zimesababisha mavuno machache zaidi ya nafaka tangu mwaka 2011 ambayo ni asilimia 70 chini ya wastani. Msemaji huyo ameongeza kuwa kama hakuna msaada wa kibinadamu, watu zaidi ya milioni 2.1 nchini Somalia watakabiliwa na njaa kali hadi mwishoni mwa mwaka huu.

  Bw. Dujjaric ameonya kuwa mpango wa muitikio wa kibinadamu wa nchi hizo mbili bado unakosa fedha. Nchini Somalia zimetolewa asilimia 45 tu ya dola bilioni 1 za kimarekani zinazohitajika, huku nchini Sudan zikitolewa asilimia 31 tu ya dola bilioni 1.1za kimarekani.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako