• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 7-Septemba 13)

  (GMT+08:00) 2019-09-20 18:20:36

  Mugabe kuzikwa Jumapili

  Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, aliyefariki nchini Singapore Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 95, umefika Zimbabwe Jumatano alasiri kabla ya mazishi yake yaliyopangwa kufanyika Jumapili, yaani hapo kesho.

  Wanasiasa akiwemo rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na mamia ya raia wamepokea mwili wa Mugabe kwenye uwanja wa ndege.

  Katika shughuli ya mapokezi katika uwanja wa ndege rais Mnangagwa alitoa risala akisifu maisha ya marehemu Mugabe, na kumwita baba wa taifa, mwalimu wa mapinduzi na nguzo ya Umoja wa Afrika.

  Rais Mnangagwa amesema, serikali ya Zimbabwe itauaga mwili wa Mugabe kitaifa tarehe 14 kwenye uwanja wa michezo wa kitaifa kabla ya mazishi yatakayofanyika Septemba 15.

  Mugabe, alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1980. Alikuwa madarakani kwa karibu miongo minne kabla ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi mwaka 2017.

  Alhamisi na Ijumaa, Mwili wa Mugabe ulilala katika uwanja wa mpira wa Rufaro eneo la Mbare mjini Harare, ambapo ndipo alipoapishwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Zimbabwe baada ya kupatiwa uhuru kutoka kwa koloni la kiingereza mwaka 1980.

  Taratibu za kitaifa za kuuaga mwili wake zilifanyika ,kwenye uwanja wenye uwezo wa kupokea watu 60,000 kabla ya kuzikwa kijijini kwao hapo kesho.

  Rais wa taifa hilo Emmerson Mnangagwa ametaja kuwa ''shujaa wa taifa'' kwa jitihada zake za kuisaidia Zimbabwe kupata uhuru wake.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako