• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 7-Septemba 13)

  (GMT+08:00) 2019-09-20 18:20:36

  Rais wa Kenya asema KDF kuimarisha juhudi za kulinda amani

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameahidi kuimarisha operesheni za kulinda amani kote duniani na jeshi la ulinzi la Kenya KDF litaendelea kuunga mkono juhudi za kutafuta amani na utulivu wa Somalia chini ya uongozi wa AMISOM.

  Akipokea gwaride la askari wapya wa KDF huko Eldoret, Rais Kenyatta amesema, hatua hii siyo tu italeta amani, usalama na utulivu kwa nchi jirani, bali pia italeta amani na usalama kwa Kenya kutokana na makundi ya kigaidi na matishio mengine. Amesisitiza kuwa askari wa Kenya wataendelea kushikilia desturi ya kushiriki kwenye operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa kila watakapohitajika.

  Ameongeza kuwa, Kenya siku zote inashirikiana na nchi zote na watu wote duniani wanaofuata kanuni za kimataifa za kuheshimu haki za binadamu, demokrasia na uhuru.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako