• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 7-Septemba 13)

  (GMT+08:00) 2019-09-20 18:20:36

  Misaada zaidi yahitajika kwa ajili ya kukabiliana na wakimbizi wa Somalia

  Baraza la Wakimbizi la Norway NRC limetoa wito kwa wafadhili kuongeza misaada ya dharura ya kibinadamu ili kusaidia kuepusha kuongezeka zaidi kwa wakimbizi nchini Somalia.

  Mkurugeni wa NRC nchini Somalia Bw. Victor Moses amesema, masuala mchanganyiko yakiwemo migogoro, ukosefu wa usalama na ukame yamewalazimisha wasomalia zaidi ya laki 2.5 kukimbia makazi yao katika miezi saba ya mwaka huu. Idadi hiyo huenda ikaendelea kuongezeka kama mashirika ya misaada yatakuwa na uhaba wa fedha.

  Habari zinasema, mwaka huu, shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa limeomba dola za Kimarekani bilioni 1.08 kwa ajili ya programu za kibinadamu nchini Somalia. Lakini mpaka sasa, zimelipwa asilimia 47 tu ya fedha.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako