• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 7-Septemba 13)

    (GMT+08:00) 2019-09-20 18:20:36

    Serikali ya Sudan na makundi ya wapiganaji wakubaliana kufanya mazungumzo ya amani mwezi ujao

    Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na baraza la utawala nchini Sudan, Serikali ya Sudan na makundi ya wapiganaji wamekubaliana kufanya mazungumzo ya amani Oktoba, 14.

    Tangazo hilo lilitolewa baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Juba kati ya wawakilishi wa serikali ya Sudan na makundi ya wapiganaji yanayotoka majimbo ya Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile, kufuatia pendekezo la upatanishi lililotolewa na rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini.

    Pande hizo pia zimekubali kuunda kamati maalumu za kupanga mazungumzo ya amani, kufuatilia utaratibu wa kuwaachia huru wahalifu wa kivita na wafungwa, kushughulikia hatua za kumaliza uhasama na kuidhinisha utaratibu wa usimamizi.

    wakati huo huo nchi tatu wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika waliomba kuondolewa vikwazo vyote vya kimataifa nchini Sudan baada ya nchi hiyo kuunda serikali ya mpito inayoongozwa na raia.

    Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa na balozi wa Cote dÍvoire katika Umoja wa Mataifa Leon Kacou Adom, nchi hizo tatu zikiwemo Cote dÍvoire, Guinea ya Ikweta na Afrika Kusini pamoja na Umoja wa Afrika zimeeleza kutaka kuondolewa kwa vikwazo vyote pamoja na kuiondoa nchi hiyo kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi.

    Taarifa hiyo pia imeeleza kwamba Baraza la Amani na Usalama la AU limeamua kuondoa vikwazo vilivyoiwekea Sudan vilivyodumu kwa miezi mitatu, kufuatia maendeleo chanya nchini humo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako