• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 7-Septemba 13)

  (GMT+08:00) 2019-09-20 18:20:36

  China yatetea utaratibu wa pande nyingi, mazungumzo na ushirikiano kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

  Mjumbe wa kudumu wa China katika ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa mjini Geneva, Uswizi Bw. Chen Xu amehutubia mkutano wa 42 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa niaba ya nchi zenye maoni yanayofanana, akifafanua maoni kuhusu mfumo wa pande nyingi katika mambo ya haki za binadamu na kazi za ofisi ya kamishna mwandamizi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

  Bw. Chen amesema hivi sasa kutokana na ongezeko la hali ya utatanishi, vitendo vya upande mmoja na kujilinda, binadamu wanakabiliwa na changamoto kubwa zaidi ya kimataifa, na dunia inahitaji zaidi utaratibu wa pande nyingi kuliko zamani.

  Bw. Chen amesema nchi zenye maoni yanayofanana zinamtaka kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na ofisi yake kufuata kanuni ya katiba ya umoja huo, na kufanya kazi kwa njia yenye haki, usawa na ya kiujenzi, bila ya kuingiza mambo ya kisiasa na kutumia vigezo tofauti. Aidha amemtaka kamishna wa haki za binadamu na ofisi yake kuhimiza pande mbalimbali kufanya mazungumzo kwa kufuata kanuni ya usawa, kuheshimiana na kunufaishana.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako