• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 7-Septemba 13)

  (GMT+08:00) 2019-09-20 18:20:36

  Waziri mkuu wa Uingereza apata uungaji mkono baada ya kura tatu tofauti za maoni kukipa chama chake ushindi

  Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepewa ushindi baada ya kura tatu tofauti za maoni kukipa chama chake cha Wahafidhina ushindi dhidi ya washindani wake.

  Ushindi huo umekuja baada ya kujiuzulu kwa waziri wa Kazi na Pensheni Amber Rudd ambaye ni mmoja wa mawaziri wake muhimu. Pia ushindi huo unakuja wakati ambao wanasiasa wanajiandaa kukutana Jumatatu kwenye Baraza la Makabwela, ambapo jaribio la pili litakuwa ni kuitisha uchaguzi mkuu. Chama kikuu cha upinzani cha Labour kimeungana pamoja na vyama vyenye viti vichache bungeni vikiwemo Liberal Democrats, Chama cha Wascotland SNP, Plaid Cymru na chama cha Green.

  Kura yao ya pamoja inamaanisha kuwa Johnson hatapata theluthi mbili ya kura ya kumuwezesha kutoa uamuzi wa kufanya uchaguzi katikati ya Oktoba, kufuatia mkutano muhimu utakaofanyika Oktoba 17 huko Brussels.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako