• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 11-Aprilii 17)

  (GMT+08:00) 2020-04-17 17:15:06
  Rais Trump adaia Marekani imefika kilele ya maambukizi mapya ya corona.

  Rais wa Marekani Donald Trump amesema nchi yake imefikia kilele cha kupata visa vipya vya ugonjwa wa COVID-19 na kutabiri kuwa baadhi ya majimbo yataondoa marufuku ya kutotoka nje na kurejea katika hali ya kawaida mwezi huu.

  Katika maelezo yake ya kila siku White House kuhusu ugonjwa huo, Rais Trump amesema muongozo mpya wa kurejelea shughuli za kawaida utatangazwa rasmi baada ya kuzungumza na magavana.

  Marekani ina takribani watu 638,000 waliothibitishwa kuwa ugonjwa wa COVID-19 na zaidi ya vifo 30,800.

  Siku ya Jumatano, Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa takwimu za kitaifa zinaashiria nchi yake imepita kilele cha maambukizi mapya ya virusi vya corona, hivyo anatumaini taifa lake litaendelea hivyo, kupiga hatua zaidi ya kuepusha maambukizi mapya mengi.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako